News

Posted date: 09-Jul-2024

Tumieni Njia Rahisi Kuupata Umeme wa Jotoardhi-Asema Katibu Mkuu Nishati Mhandisi Mramba

News Images

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba ameiagiza TGDC kuongeza jitihada katika upatikanaji wa Nishati ya Jotoardhi.

Mhandisi Mramba ameyasema hayo leo Julai 9, 2024 wakati alipotembelea maonesho ya Kimataifa ya 48 ya Sabasaba katika viwanja vya Mwalimu Nyerere akiwa katika banda la Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania TGDC.

Vilevile Mhandisi Mramba ameshauri kutumia njia rahisi itakayowezesha kupatikana kwa nishati ya Jotoardhi kwa wakati ambayo itaingizwa katika gridi ya Taifa.

Naye Meneja Mkuu wa Kampuni ya uendelezaji Jotoardhi Tanzania Mhandisi Mathew Mwangomba amemuahidi Katibu Mkuu Nishati kuwa timu ya TGDC ipo tayari kwa kutumia weledi na jitihada zote kuhakikisha Tanzania inaingia katika historia ya uzalishaji wa nishati ya jotoardhi duniani.