News

Posted date: 03-Apr-2024

"This is a perfect time for utilizing geothermal energy", Said Deputy Permanent Secretary, Ministry of Energy Visited TGDC Dr.James Mataragio Pays a

News Images

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Dkt. James Mataragio amefanya ziara ya kikazi na kuongea na Menejimenti ya Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania TGDC, kisha kusema lengo la ziara yake ni kuifahamu TGDC, miradi wanayoitekeleza pamoja na changamoto zinazowakabili huku akihimiza kampuni hiyo kuhakikisha inaisaidia Serikali kufikisha lengo lake la matumizi ya nishati safi kwa wananchi walio wengi.

Akiongea na Menejimenti ya TGDC Aprili 2, 2024 Dkt. Mataragio amesema, amefurahishwa sana na utekelezaji wa shughuli na miradi unaofanywa na TGDC na kwamba kama Serikali wapo tayari kuipa nguvu zaidi ili itemize malengo yaliyokusuduwa ya upatikanaji wa jotoardhi.

ninashukuru kwa ukaribisho, niwapongeze TGDC mnafanya kazi nzuri na mtambue yakuwa, huu ni wakati sahihi wa nchi kuwa na mtumizi ya nishati jadidifu ikiwemo ya jotoardhi. Na kwa kuwa Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ni bingwa wa nishati safi na malengo ya nchi ni kuwa na 80% ya nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034, ninaamini TGDC itatufikisha huko”, amesema Dkt.Mataragio.

Aliongeza kuwa, “nimekubali kuwa balozi wenu, nitaisemea TGDC na Jotoardhi ili wananchi na wadau wajue tunaitafuta rasilimali ya jotoardhi na ninaiona kampuni hii itakuwa kubwa Zaidi, ninawapongeza sana, Kuhusu changamoto mlizonazo nitazishughulikia pamoja na wenzangu katika Wizara”, alimaliza.

Awali akiwasilisha taarifa ya utekelezaji, Meneja Mkuu wa TGDC Mhandisi Mathew Mwangomba alinza kwa kumshukuru kiongozi huyo kwa kuitembelea TGDC, kisha kumpitisha kufahamu miradi ya kipaumbele akisema, kila mmoja kwa nafasi yake ana nafasi ya kufanikisha upatikanaji wa nishati ya umeme ambayo itaongeza uhakika wa upatikanaji wa Umeme lakini pia ni rafiki wa mazingira.

“tunashukuru kwa ziara yako nasi tunakukaribisha, tunaomba uwe balozi wetu, uisemee jotoardhi, na wengi wakiifahamu ni rahisi kusonga mbele, na maelekezo yote utakayotuelekeza, tutayatekeleza lakini zaidi, niwaombe kulitangaza Kongamano la Jotoardhi la ukanda wa Afrika (ARGeo - C10) ambalo litafanyika kuanzia tarehe 11-17 Novemba, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere”

TGDC “Tunastahili Nishati Safi