News

Posted date: 26-Feb-2024

TGDC Yatekeleza Ahadi ya Katibu Mkuu-Nishati, Mha.Mramba.

News Images

Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) imekabidhi Jezi za mpira na Fulana (T-shirt) kwa kikundi cha ngoma za asili cha Jotoardhi na timu ya mpira wa miguu ya jotoardhi katika kijiji cha Nanyala, Mkoani Songwe tqrehe 22.02.2024,kutokana naahadi ya Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba wakati alipo fanya ziara katika mradi huo.

Akikabidhi vifaa hivyo kwaniaba ya Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti Pamoja na Watumishi wa TGDC, Afisa Mkuu wa Mawasiliano Bi.Khadija Faru alisema; lengo la kukabidhi vifaa hivyo ni kuteleleza ahadi iliyotolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Mramba, aliyoitoa wakati wa ziara yake kukagua maendeleo ya mradi wa rasilimali ya Jotoardhialiyoifanya na kuagiza TGDC iwezeshe vikundi hivyo sare.

"ni jambo la kumshkuru Mungu, leo niko hapa kwaniaba ya uongozi wa TGDC kukabidhi jezi na sare mlizoahidiwa na kiongozi wetu ambaye ni Katibu Mkuu wa wizara mhandisi Felchesmi Mramba. Tunaamini mtazitunza na mtazitumia kwa lengo kusudiwa huku mkiisaidia jamii iielewe TGDC ni nini na inafanya nini", alisema Bi. Khadija.

Akiongea kwaniaba ya timu ya mpira na kikundi cha ngoma, bw Imani Juma naDaniel Jakobwalisema, wanaishukuru TGDC kwa kutekeleza ahadi aliyoitoa kiongozi na Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na kwamba, watatumia fursa hiyo kuelimisha jamii juu ya nishati ya Jotoardhi.

TGDC inaendelea kujenga mahusiano mema na jamii inayozunguka miradi inayoisimamia na kwa kufanya hivyo, hadi sasa miradi hiyo inaendelea kutekelezwa kwa uzuri kutokana na jamii kuwa karibu nayo.

TGDC, tunastahili nishati safi