News

Posted date: 26-Feb-2024

Naibu Waziri Mkuu Mheshimiwa Dk.Doto Biteko Asema-Tumeamua kwa Dhati Kuendeleza Miradi ya Jotoardhi

News Images

Tuanze na Megawati 10-Kiejo Mbaka

Jotoardhi kuongeza nguvu katika upatikanaji wa umeme

Katika kuhakikisha serikali inatatua changamoto ya upungufu wa nishati ya umeme nchini, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe.Dkt.Doto Biteko amewahakikishia wananchi kuwa, ni muda muafaka kwa serikali kuongeza upatikaji wa nishati ya umeme kupitia vyanzo mbalimbali ikiwemo nishati jadidifu ya jotoardhi.

Dkt. Biteko amesema hayo tarehe 20 Februari, 2024 mara baada ya kukagua vyanzo vya Jotoardhi vya Kiejo-Mbaka (60MW) na Ngozi (MW 70) mkoani Mbeya akifuatana na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Mbeya wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa, Juma Homera.

"Miradi hii ya Jotoardhi sasa lazima ianze, tutaanza na megawati 10 hapa Kiejo-Mbaka na Ngozi tutaanza na megawati 30 huku nyingine zikifuata” Alisema Dkt. Biteko.

pamoja na mradi ya jotoardhi, tunakwenda kuzalisha umeme wa jua, upepo, hivyo twende tukajenge vyanzo vingi, tuwe na uwanda mpana wa vyanzo ili tusipate shida, na nimshukuru Mhe.Rais.Dkt.Samia, bwawa la Mwl.Nyerere limekamilika na mashine ya kwanza inatoa umeme, tunakamilisha hatua za kuuingiza kwenye Gridi ya Taifa ili tuanze kuutumia: hivyobasi Watanzania tuvumilie ili tukamilishe”, aliongeza Mhe.Dkt.Biteko

Mhe. Dkt.Biteko alihitimisha kwa kutoa wito kwa wananchi walio kwenye maeneo yaliyo na rasilimali ya jotoardhi kutoa ushirikiano kwa serikali ili wasicheleweshe utekelezwaji wa mradi akisema kuwa yeye na Mhe.Rais wanakerwa sana na kukatika kwa umeme.

pamoja na mradi ya jotoardhi, tunakwenda kuzalisha umeme wa jua, upepo, hivyo twende tukajenge vyanzo vingi, tuwe na uwanda mpana wa vyanzo ili tusipate shida, na nimshukuru Mhe.Rais.Dkt.Samia, bwawa la Mwl.Nyerere limekamilika na mashine ya kwanza inatoa umeme, tunakamilisha hatua za kuuingiza kwenye Gridi ya Taifa ili tuanze kuutumia: hivyobasi Watanzania tuvumilie ili tukamilishe”, aliongeza Mhe.Dkt.Biteko

Mhe.Dkt.Biteko alihitimisha kwa kutoa wito kwa wananchi walio kwenye maeneo yaliyo na rasilimali ya jotoardhi kutoa ushirikiano kwa serikali ili wasicheleweshe utekelezwaji wa mradi akisema kuwa yeye na Mhe.Rais wanakerwa sana na kukatika kwa umeme.

Pia Dkt. Biteko Aliwaelekeza watendaji wa Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania (TGDC) kufanya kazi zinazoleta matokeo kwani Serikali inatafuta fedha za kutekeleza miradi hiyo na wajibu wa watendaji wa Taasisi hiyo ni kuhakikisha miradi hiyo inafanikiwa.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe.Juma Homera alisema, kama mkoa wataendelea kumuunga mkono Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha kuwa pale anapogundua chanzo chochote cha nishati ya umeme watakilinda kama ilivyo Kiejo- Mbaka na Ngozi lakini pia kuyatunza mazingira ya Mbeya na kwamba hiyo ni mipango ya mkoa huo ili jotoardhi iendelee kutamalaki mpaka hapo ambapo katizo la umeme litakuwa historia nchini, huku akizipongeza TANESCO na TGDC kwa ushirikiano zinazoutoa kwa mkoa.

Awali akitoa maelezo mafupi juu ya miradi hiyo, Meneja Mkuu wa Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania TGDC Mha. Mathew Mwangomba alisema, mradi wa Kiejo-Mbaka una lengo la kuzalisha megawati 60 ambapo awamu ya kwanza itaanza na megawati 10 na ya pili kumalizia megawati 50 zitakazobakia na kwamba endapo utakamilika utaongeza usalama wa upatikanaji wa umeme, pia ni rafiki wa mazingira na utatekelezwa kwa kufuata sharia, kanuni na taratibu zote za nchi.

Mha. Mwangomba aliongeza kuwa, uendelezaji wa miradi ya jotoardhi unapitia katika hatua za tafiti za kijiosayansi yaani Jiosayansi ya Kemia, Fizikia na Jiolojia ya eneo husika na kumhakikishia Waziri huyo kuwa vyote hivyo vimefanyika tena kwa kutumia rasilimali watu wa ndani kwa kushirikiana na mashirika ya wahisani. Vilevile, alitumia nafasi hiyo kuishukuru serikali ya Tanzania na mfuko wa maendeleo wa Umoja wa Afrika (GRMF) kwa kuwezesha upatikanaji wa fedha.

Mhandisi Mwangomba alimaliza kwa kusema, TGDC ni lazima itoe umeme.

Ziara hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali mkoa wa Mbeya,mwenyekiyi wa bodi ya TGDC, machifu, wananchi, watumishi wa wizara ya nishati pamoja na watumishi wa TGDC