News

Posted date: 21-Apr-2023

KUMBUKIZI: Meneja Mkuu Mstaafu wa kwanza wa Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC), Mhandisi Boniface Njombe

News Images

KUMBUKIZI: Meneja Mkuu Mstaafu wa kwanza wa Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC), Mhandisi Boniface Njombe akihutubia na kutoa maelezo kwenye vyombo vya habari kuhusu kongamano la Jotoardhi Tanzania liliofanyika kuanzia tarehe 25 Oktoba hadi 2 Novemba mwaka 2014 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC),Tanzania. Kongamano hilo lilijulikana kama FIFTH AFRICAN RIFT GEOTHERMAL CONFERENCE.

Lengo kuu la mkutano huo lilikuwa ni kuonyesha mafanikio yanayojitokeza kuhusu maendeleo ya jotoardhi barani Afrika. Pia ililenga kukuza ushirikiano wa kikanda na kutoa jukwaa bunifu la kubadilishana taarifa kuhusu utafutaji, maendeleo, uwekezaji na matumizi ya rasilimali za jotoardhi katika kanda na kwingineko duniani.

Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa kongamano kama hili Novemba, 2024 litakalofanyika jijini Dar es Salaam, ambalo litafahamika kama 10TH AFRICAN RIFT GEOTHERMAL CONFERENCE.

TGDC, Tunastahili Nishati Safi kwa Watanzania na dunia kwa ujumla.

Endelea kutembelea mitandao yetu ya jamii kwa taarifa mbalimbali kuhusu jotoardhi.