News

Posted date: 25-May-2024

Karibuni Mpate Elimu ya Jotoardhi Katika Maonesho ya Mbeya City Expo 2024

News Images

Katika kutekeleza sera zake, Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania TGDC imeshiriki maonesho ya pili biashara ya kimataifa ya Mbeya City Expo 2024 yanayofanyika katika uwanja wa Uhindini Jijini Mbeya ambayo yatadumu kwa siku nane kuanzia tarehe 23 Mei, 2024.

Katika maonesho hayo ambayo yamefunguliwa rasmi tarehe 24 Mei, 2024 na mkuu wa mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Juma Homera ambaye amemwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara, TGDC inayatumia kutoa elimu kwa wananchi na wakazi wa Mbeya juu ya uelewa wa Kampuni na shughuli inazozifanya pamoja na kutoa elimu juu ya upatikanaji wa Nishati jadidifu ya jotoardhi.

Hata hivyo, wananchi waliotembelea banda la TGDC walionesha kustaajabishwa na sayansi inayotumika katika upatikanaji wa Nishati hiyo ya jotoardhi.

Hivyo kupitia maonesho ya Mbeya City Expo 2024, TGDC inawakaribisha wananchi kuja kupata elimu ya jotoardhi.