News

Posted date: 26-Feb-2024

Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) Yatekeleza CSR kwa Vitendo

News Images

Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC), imetoa Elimu, Msaada wa Daftari na Mabegi kwa wanafunzi katika Shule ya Msingi Mbeye 1 kuhusu rasilimali ya Nishati Jadidifu ya Jotoardhi itakayopatikana katika mradi wa Ngozi uliyopo katika Kata ya Isongole, Kijiji cha Mbeye 1, Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya.

Mradi huo wa Ngozi, unatarajiwa kuzalisha Megawati 70 za Nishati ya umeme wa Jotoardhi ambapo kwa sasa upo katika maandalizi ya hatua ya uchorongaji wa visima vya jotoardhi

Aidha, TGDC imekabidhi Tenki la Maji ujazo wa Lita 10,000 ili kuondoa adha waliyokuwa wakiipata wanafunzi wa shule hiyo, ambapo hapo awali waliyafuata maji ng'ambo ya barabara, hali iliyokuwa ikihatarisha usalama wao kwani wengine walipata ajali walipokuwa wakivuka upande wa pili.

TGDC imefanya tukio hilo ikiwa ni utekelezaji wa takwa la kisheria la uwajibikaji wa kampuni kwa jamii (CSR) kwa kuwa shule hiyo ipo katika kijiji ulipo mradi wa Ngozi na kwa kufanya hivyo, TGDC inaendeleza mahusiano mema baina yake na jamii inayozunguka eneo ulipo mradi