News

Posted date: 07-Jun-2024

KAMISHNA LUOGA AFUNGUA WIKI YA NISHATI MBADALA -TANZANIA

News Images

Kamishna wa umeme na nishati jadidifu kutoka wizara ya nishati mhandisi Innocent Luoga amefungua rasmi mkutano wa 15 wa Chama cha Wadau wa Nishati Jadidifu (TAREA) ulioambatana na wiki ya kwanza ya Nishati Jadidifu iliyoanza tarehe 4 Juni, 2024 hadi tarehe 7 Juni, 2024 wa siku mbili kuanzia tarehe 6 Juni, 2024 ujulikanao kama Wiki ya Nishati Mbadala, ambapo amesisitiza juu ya ufanikishaji nia ya serikali katika kufikia 80% ya matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Akizungumza na wadau mbalimbali walioshiriki mkutano na wiki hiyo baada ya kupita kwenye vizimba vya maonesho hayo Juni 6, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa mwl.Julius Nyerere (JNICC), Mhandisi Luoga amesema, matumizi ya nishati safi yataondoa changamoto mbalimbali zinazowakumba watanzania wengi hususan wanawake.

“matumizi ya nishati safi yataimarisha uchumi kwa kupunguza muda unaotumika kutafuta kuni na mkaa kama vyanzo vya nishati ya kupikia, jambo linalochelewesha ukuaji wa uchumi. Vilevile, tutaondokana na changamoto ya uharibifu wa mazingira tutakapotumia nishati safi kwani upatikanaji mkaa na kuni hutokana na ukataji hovyo wa miti ambao ni uharibifu wa mazingira, jambo linaloweza kuchangia vilevile mabadiliko ya tabianchi” amesema mhandisi Luoga.

Ameongeza kuwa, afya ya wananchi italindwa endapo kutakuwa na matumizi ya nishati safi ya kupikia kwani, kwa matumizi ya nishati isiyosafi hupelekea magonjwa ya kupumua na macho. Si hivyo tu, unyanyasaji mwingi umekuwa ukitokea kutokana na mazingira ya matumizi ya nishati isiyo safi kama utafutaji wa kuni na mkaa unaopelekea kuchelewesha shughuli nyingi na hivyo wanawake wengi kukumbana na adha ya unyanyaswaji kutokana na matokeo ya matumizi ya nishati isiyo safi, na ndiyo maana mkakati wa matumizi ya nishati safi yanahimizwa.

Mhandisi Luoga alihitimisha kwa kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kufuatia

Akiongea akiwa kwenye banda la maonesho la kampuni ya uendelezaji jotoardhi Tanzania (TGDC), Meneja Mkuu wa kampuni hiyo mhandisi Mathew Mwangomba alitumia fursa hiyo kueleza juu ya miradi inayoendelea kutekelezwa na pia kuwaalika katika kongamano la kikanda la jotoardhi Afrika (ARGeo-C10).

Amesema, “kwa sasa TGDC ina miradi yake mitano (5) ya kipaumbele ambayo inalenga kuzalisha MW 200. Miradi hiyo ni Ngozi 70MW (Mbeya) ambapo katika mradi huu tunaendelea kukamilisha taratibu za kuanza uhakiki wa rasilimali ya jotoardhi, Kiejo-Mbaka 60MW (Mbeya), Natron 60MW (Arusha), Songwe 5MW – 38 MW (Songwe) na Luhoi 5MW (Pwani) ambapo tunaishukuru Serikali kutuwezesha kununua Mtambo wa kuchoronga visima vya utafiti vya jotoardhi. Mtambo huu umegharimu Zaidi ya bilioni 13 na utatumika kuchoronga katika mradi wa Ngozi na katika miradi mbalimbali ya jotoardhi nchini”