Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania

Tanzania Geothermal Development Company

(TGDC)

Uhusiano na Wadau

Tangu kuanzishwa kwake TGDC imeanzisha uhusiano mbalimbali wa kitaasisi, kibiashara na kitaaluma na wadau wa nchini na nje.

 • Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Icelend (ICEIDA) na Mfuko wa Maendeleo wa Nchi za Nordic (NDF) – zinasaidia utafiti na utafutaji jotoardhi wa nchi kavu wa Luhoi mkoa wa Pwani na Mbaka Kiejo (mkoa wa Mbeya).
 • Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) – utekelezaji wa Programu ya Kuzidisha Nishati Jadidifu (SREP) Tanzania.
 • Kampuni ya Maendeleo ya Jotoardhi (GDC), Kenya – ushirikiano katika tathmini ya rasilimali za jotoardhi,utafiti na uchimbaji.
 • Shirika la Uhusiano wa Kimataifa la Japan (JAICA) – kujenga uwezo na mitambo ya uzalishaji umeme.
 • Mfuko wa Maendeleo ya Jotoardhi katika Bonde la Ufa la Afrika (ARGeo/UNEP) – Uchunguzi wa kina wa nchi kavu katika utafutaji, kujenga uwezo na utandaishaji.
 • Mpango wa Msaada wa Usimamizi wa Sekta ya Nishati wa Benki ya Dunia (ESMAP) – kujenga uwezo wa kufanya uchimbaji wa majaribio na ESIA katika eneo la Ngozi,
 • Mfuko wa Kupunguza Hatari katika Miradi ya Jotoardhi (GRMF) – Kugharamia kwa pamoja utafiti wa kina wa ardhini katika eneo la Kisaki na programu ya uchimbaji wa majaribio wa eneo la Ngozi.
 • Mfuko wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza (DFID)/Mfuko wa Nishati ya Jotoardhi Afrika Mashariki (EAGER) – Uendelezaji wa vifano vya biashara.
 • Taasisi ya Sayansi za Ardhi na Maliasili ya Ujerumani (BGR) – utafiti wa ardhini Meru na Natron.
 • Toshiba – Waraka wa Maelewano (MOU) wa kuleta mtambo wa juu ya kisima wa kudhibiti jotoardhi (well head unit).
 • Chuo Kikuu cha Dodoma – Waraka wa Maelewano (MOU) - kujenga uwezo kwa ajili ya utafiti na maendeleo.
 • Wakala wa Utafiti wa Kijiolojia Tanzania (GST) – Waraka wa Maelewano (MOU) – maelewano ya ushirikiano katika sayansiardhi.
 • Chuo cha Madini Dodoma – Waraka wa Maelewano (MOU) wa Ushirikiano katika kujenga uwezo wa kuwafunza mafundi sanifu.
 • Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (inayoendelea) – Waraka wa Maelewano (MOU) - katika ushirikiano wa utafiti na maendeleo.