Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania

Tanzania Geothermal Development Company

(TGDC)

Mazingira na Jamii

Sheria na sera: TGDC inazingatia sheria na sera zilizomo kulinda ustawi wa mazingira na jamii zinazozunguka maeneo ya miradi. Ifuatayo ni orodha ya hati za taifa na kimataifa kama miongozo ya utendaji kijamii na kimazingira.

Sera ya Taifa ya Mazingira, 1997

Sera ya Taifa ya Mazingira ipo kuhakikisha miradi yoyote inayoanzishwa inatekelezwa kiuendelevu kiuchumi wakati huo ikilinda masuala ya mazingira na jamii kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho. Mpango wa Taifa wa Mazingira unataka Tathmini ya Athari kwa Mazingira (Environmental Impact Assessment) (EIA) iwe ni lazima kwa miradi yote ya maendeleo yenye uwezekano wa kuleta athari kwa mazingira.

Sera ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (2001)

Lengo la sera hiyo ni kuzuia maambukizo ya UKIMWI ambayo ni janga la kitaifa na kimataifa. Ni tishio kubwa kwa ukuaji na maendeleo ya taifa. Kupambana dhidi ya janga hili kunashirikisha watumishi wa afya, viongozi wa kisiasa, asasi sizizo za kiserikali, watu wanaoshi na virusi vya VVU/UKIMWI, viongozi wa jamii , familia na mtu mmoja mmoja.

Sera ya Wanyamapori na Maeneo Oevu ya Tanzania, 2007

Sera ya Wanyama Pori na Maeneo Oevu ya Tanzania inahimiza uhifadhi wa wanyamapori kama maliasili. Pia inahimiza mazingira safi, kuboresha hali ya hewa, uhifadhi wa maji na udongo. Kutokana na shughuli za binadamu kwa ajili ya maendeleo yao kwenye rasilimali za wanyamapori ndani na nje ya maeneo yaliyotengwa, Sera inahimiza tathmini ya mazingira kwa ajili ya maendeleo yanayopendekezwa ili kupunguza madhara.

Sera ya Taifa ya Misitu, 1998

Lengo la jumla la Sera ya Taifa ya Misitu (URT), 1998 ni kuzidisha mchango wa sekta ya misitu kwa maendeleo endelevu ya Tanzania na kuhifadhi na usimamizi wa maliasili zake.

Sera ya Utwaaji Ardhi na Upatiaji Makazi Mapya

Hakuna Sera ya Upatiaji watu makazi mapya nchini Tanzania. Kutokana na hali hiyo mchakato wa upatiaji watu makazi mapya unaongozwa na Sheria ya utwaaji Ardhi ya 1997, Sheria ya Ardhi ya 1999 na Kanuni za Ardhi za mwaka 2001. Mswada wa muundo wa Sera ya Upatiaji Makazi ya Taifa uliotayarishwa 2003 kwa kuzingatia mapendekezo ya Benki ya Dunia, OP 4.12 kuhusu kuhamishwa kwa nguvu inasema kwamba:

1. Uhamishwaji kwa nguvu lazima uepukwe au upunguzwe sana kadri iwezekanavyo kwa kutafuta maeneo mbadala yenye kufaa.

2. Kama haiwezekani, shughuli za uhamishwaji ni lazima zipangwe na kutekelezwa kama programu za maendeleo endelevu ili kuwanufaisha waliohamishwa .

3. Watu walioondoshwa kwenye makazi yao ni lazima washauriwe kwa ukamilifu na washiriki katika kupanga na kutekeleza mipango ya upatiwaji makazi.

4. Watu walioondoshwa kwenye maeneo yao ni lazima wasaidiwe katika kuboresha njia zao za kujipatia kipato na maisha bora angalau kufikia maisha ya kabla hawajahamishwa.

Sera za Kulinda za Benki ya Dunia

Taasisi nyingi za fedha za kimataifa zinachukua hatua za dhati za kuhakikisha kuwa mikopo wanayozipa nchi au sekta binafsi haiathiri mazingira. Kundi la Benki ya Dunia likiongozwa na seti ya sera na taratibu jumuishi, hushughulikia malengo na madhumuni makuu ya Benki kwa maendeleo. Mipango ya maendeleo iliyopendekezwa itachochea Sera za Uendeshaji za Benki ya Dunia zifuatazo:

1. Tathmini ya Mazingira (OP 4.01, BP 4.01, GP 4.01)

2. Makazi ya Mazingira ya Asili (OP 4.04, BP 4.04, GP 4.04)

3. Urithi wa Maumbile ya Kitamaduni (OP/BP 4.11)

4. Misitu (OP 4.36, GP 4.36)

SHERIA ZA TAIFA
Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Na. 20 (2004) (au Sura 191)

Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Sura ya 1991 ndio sheria kuu inayodhibiti usimamizi wa mazingira nchini. Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (EMA) inatambua “…haki ya kila raia kuishi katika mazingira safi, salama na yenye afya, na haki ya upataji wa rasilimali za kimazingira kwa ajii ya burudani, elimu, afya , dini/kiroho, utamaduni na madhumuni ya kiuchumi”.

Kanuni za Tathmini na Ukaguzi Wa Athari za Mazingira (2005)

Kanunin za Tathmini na Ukaguzi wa Athari za Mazingira Na. 349 za mwaka 2005 zilitayarishwa kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004. Kanuni hizi zinatoa msngi wa kufanya tathmini na ukaguzi wa athari za mazingira kwa miradi mbalimbali ya maendeleo.