Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania

Tanzania Geothermal Development Company

(TGDC)

Historia ya Jotoardhi

Historia ya jotoardhi Tanzania inaenda hadi enzi za mwanzoni za Uchifu, hususan eneo la Mtagata Wilaya ya Kyerwa, Mkoani Kagera ambapo watu walimlipa Chifu wa Karagwe ada kwa kuoga; ada hii ilipunguzwa kwa miaka kadhaa baada ya Wajerumani kutawala, na hatimaye ilijafutwa kabisa na mamlaka ya Wajerumani (Grant C.H.B.). Bado inasemwa kuwa chemchemu hizi za maji moto zina nguvu ya uponyaji kwa aina zote za vitisho, vidonda, magonjwa ya zinaa na wenyeji bado wanatumia madimbwi haya.

Kimsingi, historia ya jotoardhi ni matumizi ya moja kwa moja ya rasilimali, hivi sasa TGDC inafanyia kazi matumizi ya rasilimali hiyo kwa kuzalisha umeme na kuendeleza matumizi ya moja kwa moja kwenye kilimo na viwanda vya kati na vikubwa.