Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania

Tanzania Geothermal Development Company

(TGDC)

Matumizi ya moja kwa moja ya Jotoardhi

Ili kutumia kikamilifu rasilimali ya jotoardhi, TGDC inaendeleza matumizi ya moja kwa moja ya nishati ya jotoardhi kuboresha maisha ya Watanzania kupitia vyanzo rahisi vya nishati. Kama ilivyo kwenye Kielelezo, nishati ya joto iliyo kwenye maji ya moto yaliyokifu chumvi, yana matumizi mengi kutegemeana na joto na kemia ya maji na shughuli nyingine mahususi za eneo za kiuchumi na kijamii.TGDC TGDC imefanya utafiti wa kuanzisha miradi ya majaribio ya matumizi ya jotoardhi moja kwa moja katika maeneo ya Ngozi na Kisaki. Maeneo ya awali ya matumizi kiuchumi yanajumuisha kupasha joto nyumba za vioo za kuhifadhi mimea (greenhouse), kukausha nafaka, ufugaji wa samaki, michakato ya viwandani, kupoza na kupasha joto hewa na nyingine. Matokeo haya yanatia moyo na Kampuni inapanga kufanya upembuzi yakinifu wa awali ikiwa ni pamoja na kufahamu kiufundi uwezo wa soko la rasilimali pamoja na mazingira na kijamii. Kwa siku za baadaye TGDC inakusudia kutumia Serikali, taasisi za utafiti, wajasiriamali na sekta binafsi kwa jumla ikiwemo taasisi za kibiashara kujadili fursa za matumizi zilizopo na namna ya kushirikiana kutumia uwezo huo.