Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania

Tanzania Geothermal Development Company

(TGDC)

Uzalishaji Umeme

Mitambo ya umeme hutumia mvuke kutoka hifadhi za jotoardhi kuzalisha umeme. Kuna teknolojia za aina tatu ya mitambo ya umeme inayotumiwa kugeuza vimiminika kuwa umeme – mvuke mkavu, kimiminika kinachokaribia kuwa mvuke na mzunguko jozi. Aina ya ugeuzaji inayotumiwa (inateuliwa wakati wa uendelezaji) inategemea hali ya kimiminika (mvuke au maji) na kiasi cha joto lake.
Katika usanifu rahisi kabisa, unaojulikana kama mvuke mkavu, mvuke unaenda moja kwa moja kupitia tabo (turbine) halafu kwenye kondensa ambako mvuke hugeuzwa kuwa maji. Njia ya pili ni maji yenye joto kali hupunguzwa mgandamizo (depressurized or flashed) na kuwa mvuke unaotumika kuendesha tabo. Mitambo ya kutumia mvuke wa ‘flash’ ndiyo inayojulikana zaidi. Inatumia jotoardhi la hifadhi za maji yenye joto zaidi ya nyuzijoto 360°F (182°C).
Njia ya tatu inaitwa mfumo wa mzunguko wa jozi (binary cycle system), maji ya moto hupitishwa kwenye kibadili cha joto (heat exchanger) ambapo inapasha joto kimiminika cha pili kama ‘isobutene’ kwenye mzunguko uliozibwa pande zote. Isobutene inachemka kwenye joto la chini zaidi kuliko maji, kwa hiyo ni rahisi kugeuzwa kuwa mvuke wa kuendesha tabo. Mitambo ya nishati ya mzunguko wa jozi inaendeshwa na maji yenye joto la chini la kiasi cha 225°-360°F (107°-182°C).
Aina hizo tatu za mitambo ya jotoardhi, yote huvuta maji moto na mvuke kutoka ardhini, kutumia na halafu kurejesha yakiwa maji vuguvugu kuendeleza uhai wa chanzo cha joto.