Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania

Tanzania Geothermal Development Company

(TGDC)

Kampeini ya uelimishaji

TGDC tayari inafahamisha jamii ya Tanzania na Serikali za Mitaa kuhusu manufaa ya jotoardhi na kero zao, Kata 19 za eneo la utafutaji la Ngozi Mkoa wa Mbeya na Kisaki mkoani Morogoro ikiwemo wafanyakazi na menejimenti ya Pori tengevu la Seleous wanatambua jitihada za taifa za kuendeleza rasilimali za jotoardhi nchini.
Kampeni za TGDC zinalenga kujenga uelewa wa jamii na kuongeza muonekano wa TGDC katika maeneo yaliyolengwa na zaidi. Nishati ya jotoardhi ni tasnia mpya nchi Tanzania na watu wengi hawaelewi kuhusu teknolojia hii na kampuni mpya iliyoanzishwa na Serikali kwa madhumuni ya kuharakisha maendeleo ya nishati hii na kuinusuru nchi na matatizo ya kukatika kwa umeme. . Kwa hiyo madhumuni ya kampeni za utambuzi ni pamoja na:

  • Kuitambulisha kampuni (TGDC) na majukumu yake,
  • Kuongeza uelewa wa teknolojia ya jotoardhi, shughuli zake, manufaa ya kiuchumi na kijamii na kero zao,
  • Kutoa fursa ya mawasiliano baina ya waendelezaji wa mradi wa jotoardhi na jumuiya inayozunguka mradi,
  • Kuelimisha na kushirikisha jamii katika kushughulikia athari za kijamii na mazingira zinazotokana na mradi wa jotoardhi,
  • Kuongeza uelewa wa jamii kuhusu fursa za matumizi ya moja kwa moja ya jotoardhi zaidi ya kuzalisha umeme.

Njia ya kufanya kampeni hii ni kwa ushauriano na watu wenye shauku na wanaoguswa, kukusanya maoni, na mapendekezo kutoka kwao kupitia vikundi vya majadiliano na kamati za maendeleo ya kata zilizobainishwa (WDC) na mikutano ya hadhara katika eneo la mradi.