Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania

Tanzania Geothermal Development Company

(TGDC)

Kuhusu TGDC

Kampuni ya Maendeleo ya Jotoardhi Tanzania (TGDC) ni kampuni tanzu ya kampuni ya Ugavi wa Umeme Tanzania-(TANESCO), inayomilikiwa na Serikali ya Tanzania kwa 100%. Kampuni hii imeanzishwa Desemba 2013 kwa madhumuni ya kusimamia na kuongoza maendeleo ya jotoardhi nchini Tanzania. Kampuni ilianza rasmi shughuli zake Julai 2014 kwa jukumu na mamlaka ya kutafiti, Kuchimba na kutumia rasilimaliza jotoardhi kwa uzalishaji umeme na matumizi mengine ya moja kwa moja.

Sababu ya Kuanzishwa TGDC: Kwa miongo mingi Tanzania imekabiliwa na upungufu wa uzalishaji wa umeme wa kutosha kutokana na sababu
mbalimbali. Serikali imechukua hatua mbalimbali za kutanzua tatizo la mgao wa umeme, ambapo baadhi yahatua hizo ni ghali sana na zimeathiri sana mazingira. Ili kuepuka kujirudiarudia kwa matatizo haya. Serikali imeamua kuwa na vyanzo mbalimbali vya uzalishaji waumeme vya nishati JADIDIFU vikiwemo Jua, Upepo na JOTOARDHI.