Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania

Tanzania Geothermal Development Company

(TGDC)

Mkutano wa 5 wa Kimataifa wa Jiolojia, Ubeljiji (GB2016)

26/02/2016 - 29/02/2016

MUDA: 21:00

Mahali: Mons, Belgium

HADHIRA:000

Mkutano wa Kimataifa wa Jiolojia wa Ubeljiji , 2016 umeandaliwa chini ya kaulimbiu “Mama Ardhi”. Mada mbalimbali za fani mbalimbali za Sayansi ya Udongo zitajadiliwa wakati wa mkutano, ikiwa ni pamoja na elimu ya hali ya hewa ya zamani (paleoclimatology), nishatiardhi (geoenergy) na mlimbiko, haidrolojia, nyenzo zilizoko ardhini (geomaterials), jiolojia ya miamba madini, mazingirardhi (geoenvironment,) majanga ya ardhi (geohazards, michakato ya kina ya jiolojia, elimu ya matabaka ardhini (stratigraphy) na jiolojia ya mashapo, maisha ya awali na ya zamani,, uhamaji wa matabaka ya ardhi (plate tectonics), muundo wa jiolojia, uridhiardhi (geoheritage), elimuardhi na akilojia ya ardhi. Kwa vile mada kuu ya mkutano ni “Mama Ardhi” tutajitahidi kuweka mkazo kwenye mada zinazohusiana na mazingira, rasilimali na maisha ya kale.

Ziara ya kijiolojia itafanywa kwenye machimbo ya chini ya ardhi ya La Malogne huko Cuesmes. Mwishowe matukio mbali mbali ya kisayansi yatatayarishwa wakati wa mkutano:

Sherehe ya utoaji Tuzo ya Andre Dumont 2016

Sherehe ya utoaji Tuzo ya Vandenbroeck 2016

Mkutano

Mkuu wa Wanachama wa Geologica Belgica 2016

Kwa habari zaidi bonyeza hapa


Mkutano wa 5 wa Kimataifa wa Jiolojia, Ubeljiji (GB2016)